Tuesday, July 28, 2009

Yaaani Uswazi Noma!!


Duuu kweli uswazi noma kwani yanii watu wanakula kideo bure hadi noma

na mpaka watu wazima wamecha kazi kweli hii kiboko wadau wetu?

Monday, July 27, 2009

Hii ndio daladala Bwana!

Nilikuwa natokea Bagamoyo nikielekea Dar/Tegeta, hivi karibuni .tulipofika eneo la Bunju,abiria mmoja alipakia mizigo ya madafu,mafenesi na mkaa.Konda bila kujali alisukumiza mizigo hiyo katikati ya miguu ya abiria.kufika kituo cha Boko,abiria zaidi wakajazana na hivyo mizigo ile ikawa kero kubwa zaidi kwa abiria.Abiria mmoja kijana alilalamika kwa kusema,”mbona mnatuumiza na haya madubwana yenu?”kumbe mwenye huo mzigo aliokua akiulalamikia huyo kijana ulikua wa mama mmoja mtu mzima wa haja.Yule mama alisema ‘koma wee mwana,hayaitwi madubwana,ni mafenesi.’Halafu aliendelea,kama ni madubwana unayo mwenyewe,huyaoni.Abiria kwenye basi walishikwa na butwaa kwa kusikia maneno kama yale yakitoka kwa mama wa makamo yale.Konda hakunyamaza,kwani alitishia kumshusha mama yule.kwa kufanya hivyo alikua amewasha moto,mama ilsema,jaribu uone hata wewe sikuogopi,’Halafu,alionesha mshangao na kusema.Kwanza nakujua,mwana haramu wa Zinga wee.Baba yako unamjua?Humjui,kwa taarifa yako,ana dubwana kama hili fenesi.Katoroka kupasuliwa Hospitali ya Tumbi mara mbili.Na kazi hii ya ukonda uiheshimu,vinginevyo ungeshachomwa moto,maana ukoo wenu mlilogewa wizi.’Ilionekana kama anasema kweli na basi lilitulia kabisa,hakukua na ushabiki.Yule konda naye akaachwa mdomo wazi,pengine kwa kubaini kwamba,bibi alikua anamjua vilivyo.Ili kuua soo kama watoto wa mjini wanavyosema,yule konda alimwambia yule kijana aliyelalamika awali kuhusu madubwana. ‘Wewe unalalamika nini,hujui kua hili ni basi la shamba .’Ilibidi abiria waangue kicheko kwa kujihami kule.Wakati huo nilikua nimefika kituo cha basi cha Tegeta.Nilishuka nikiacha bado kukiwa na kitete jambo lile.Siku hizi naogopa kuwasemesha watu hovyo,kwani hujui nani ankujua na ni nani hukujui.
Mwakyembe ajitoa mhanga


Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe ameitaka Serikali iufunge mara moja mgodi wa dhahabu wa North Mara ili sumu inayodaiwa kutoka hapo isiendelee kuwadhuru wananchi. Mbunge huyo pia ametaka mgodi wa dhahabu wa Geita ufungwe kwa sababu, za kiafya.
Jk urges police officers to go for cyber technology training


President Jakaya Kikwete has underscored the need for police to be trained in cyber technology to enable them fight fraud and other international organized crimes.
Kikwete made the call on Thursday when closing training for police officers held at the Tanzania Police Academy in Dar es Salaam.
He said international gangs were using the latest technology in committing crimes, adding that police need to be conversant with cyber technology or else criminals would outsmart them.
The president said it was imperative for police to be equipped with the latest technology through training to counter methods of organized crimes.
He said organized criminals always take advantage of police laxity to commit crimes.
The president said he was aware that police were ill-equipped, but said that the government would continue to equip them so that they can fight crime.
President Kikwete promoted 291 police officers who graduated the training to the rank of Assistant Superintended of Police, and urged them to be honest to the country and avoid taking bribes.
Speaking earlier on the Inspector General of Police Said Mwema said the Police Force was determined to work professionally to fight crimes.
Duuu hayo ndio Maisha ya mama zetu





Wete women selling snacks at the market to earn income as caught by our roving photographer recently in Pemba