
Hi kweli tulikuwa kama hawa?
ukosefu wa maji katika mtaa huo.
la Bunju,abiria mmoja alipakia mizigo ya madafu,mafenesi na mkaa.Konda bila kujali alisukumiza mizigo hiyo katikati ya miguu ya abiria.kufika kituo cha Boko,abiria zaidi wakajazana na hivyo mizigo ile ikawa kero kubwa zaidi kwa abiria.Abiria mmoja kijana alilalamika kwa kusema,”mbona mnatuumiza na haya madubwana yenu?”kumbe mwenye huo mzigo aliokua akiulalamikia huyo kijana ulikua wa mama mmoja mtu mzima wa haja.Yule mama alisema ‘koma wee mwana,hayaitwi madubwana,ni mafenesi.’Halafu aliendelea,kama ni madubwana unayo mwenyewe,huyaoni.Abiria kwenye basi walishikwa na butwaa kwa kusikia maneno kama yale yakitoka kwa mama wa makamo yale.Konda hakunyamaza,kwani alitishia kumshusha mama yule.kwa kufanya hivyo alikua amewasha moto,mama ilsema,jaribu uone hata wewe sikuogopi,’Halafu,alionesha mshangao na kusema.Kwanza nakujua,mwana haramu wa Zinga wee.Baba yako unamjua?Humjui,kwa taarifa yako,ana dubwana kama hili fenesi.Katoroka kupasuliwa Hospitali ya Tumbi mara mbili.Na kazi hii ya ukonda uiheshimu,vinginevyo ungeshachomwa moto,maana ukoo wenu mlilogewa wizi.’Ilionekana kama anasema kweli na basi lilitulia kabisa,hakukua na ushabiki.Yule konda naye akaachwa mdomo wazi,pengine kwa kubaini kwamba,bibi alikua anamjua vilivyo.Ili kuua soo kama watoto wa mjini wanavyosema,yule konda alimwambia yule kijana aliyelalamika awali kuhusu madubwana. ‘Wewe unalalamika nini,hujui kua hili ni basi la shamba .’Ilibidi abiria waangue kicheko kwa kujihami kule.Wakati huo nilikua nimefika kituo cha basi cha Tegeta.Nilishuka nikiacha bado kukiwa na kitete jambo lile.Siku hizi naogopa kuwasemesha watu hovyo,kwani hujui nani ankujua na ni nani hukujui.
e has underscored the need for police to be trained in cyber technology to enable them fight fraud and other international organized crimes.